Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Mwanza na kufungua miradi minne inayolenga kuboresha uchumi wa nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema rais ambaye atafanya ziara leo na kesho, ataongozana na viongozi wengine hadi katika Daraja la Furahisha na kulizindua.
Daraja hilo limejengwa ili kurahisisha mawasiliano kati ya waenda kwa miguu na vyombo vya moto.
Mkuu huyo wa mkoa alisema baadaye rais ataelekea Nyakato wilayani Nyamagana kufungua Kiwanda cha Sayona Drinks Limited na kuhitimisha ziara kwa siku hiyo.
Kesho Jumanne, rais atafungua Kiwanda cha Victoria Moulders and Polybags, kilichopo Igogo jijini Mwanza.
Alisema siku hiyo hiyo, ataelekea Buhongwa kwa ajili ya kufungua Kiwanda cha Dawa cha Prince Pharmaceutical Industry.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza aliomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau wengine ili kufanikisha ziara ya Rais Magufuli.
“Naamini mkoa wetu umejaaliwa amani na ulinzi wa kutosha, hivyo basi, sitarajii kusikia ripoti yeyote ya utovu wa nidhamu,” alisema Mongella.

No comments:
Post a Comment