KOREA KASKAZINI YAFUNGUA MAWASILIANO YA SIMU NA KOREA KUSINI....NI KATIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA MSIMU WA BARIDI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 3, 2018

KOREA KASKAZINI YAFUNGUA MAWASILIANO YA SIMU NA KOREA KUSINI....NI KATIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA MSIMU WA BARIDI



Korea Kaskazini imefungua tena mawasiliano ya simu na Korea Kusini ili kuanzisha mazungumzo kuhusu kushiriki kwake katika mashindano ya msimu wa baridi. Korea Kusini imethibitisha kuwa ilipata simu kutoka Kaskazini leo Jumatano.

Hii ni baada ya Kim Jong un kusema kuwa ataanzisha mazungumzo na Korea Kusini kuhusu kutumwa timu kwa mashindano ya msimu wa baridi huko Korea Kusini. Mataifa hayo mawili hayajafanya mazungumzo ya juu tangu Disemba mwaka 2015

Mwaka uliofuatia Korea Kaskazini ilikata mawasiliano na kuacha kupokea simu kwa mujibu wa maafisa kutoka Kusini Afisa kutoka Korea Kaskazini alitangaza kufunguliwa laini hiyo ya simu kwenye ujumbe uliopeperushwa mapema Jumatano.

Mkuu wa idara ya mawasiliano ya raia wa Korea Kusini Moon Jae-in, alisema kuwa kufunguliwa kwa laoni hiyo ya simu kuna umuhimu mkubwa "Inabuni mazingira ambapo mawasiliano yatakuwa rahisi kila mara," alisema.


#BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages