MBUNGE AITAKA SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI WATUMISHI WALIOISHIA DARASA LA SABA....ASEMA SERIKALI ISIPOFANYA HIVYO BASI IWATIMUE NA WABUNGE WENYE ELIMU HIYO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 7, 2018

MBUNGE AITAKA SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI WATUMISHI WALIOISHIA DARASA LA SABA....ASEMA SERIKALI ISIPOFANYA HIVYO BASI IWATIMUE NA WABUNGE WENYE ELIMU HIYO



Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma (CCM), ameitaka serikali irudishe kazini watumishi wa darasa la saba iliowafukuza vinginevyo wabunge wenye elimu ya darasa la saba pia waondolewe bungeni.

Musukuma amesema hayo bungeni Mjini Dodoma jana Ijumaa Aprili 6, alipokuwa akichangia hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema wabunge wakishaondolewa bungeni warudishwe kwa Viti Maalumu kama ilivyo kwa wanawake na walemavu ili wawatetee darasa la saba wenzao.

Musukuma amesema hotuba ya Waziri Mkuu inaonyesha mwaka wa fedha uliopita waliojiunga na darasa la saba ni milioni mbili na walioingia sekondari ni 500,000 jambo linalomaanisha wenye elimu ya darasa la saba ni zaidi ya asilimi 80.

“Serikali isiposikia kilio chetu na kuwarudisha kazini watumishi hao na wabunge wa kambi zote kuungana na kutetea watumishi hao waliofukuzwa kazi basi tutakutana 2020,” amesema Musukuma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages