Usiku wa jana Jumamosi ya Oktoba 28 msanii wa vichekesho hapa nchini Lucas Mhuvile maarufu kama Joti amefanya sherehe ya kufana baada ya kufunga ndoa takatifu na mke wake Tumaini.
Sherehe hiyo ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ilikuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia luninga ya Sinema Zetu chaneli namba 103 ya Azam Tv. Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wasanii mbalimbali wa muziki na filamu hapa nchini msanii Jackline Wolper naye pia alinaswa na kamera za ukumbi huo.
Wolper wakati akihojiwa na mtangazaji wa Sinema Zetu bwana Timothy Chelula alifunguka jinsi ambavyo amefurahishwa na hatua ya Joti kufunga ndoa na pia hakusita kueleza jinsi alivyositisha safari ya kwenda China na badala yake akaamua kuja kwenye party hiyo ya usiku wa Joti na mke wake Tumaini.
"Ni hatua nzuri kwa msanii Joti kufunga ndoa...nime-cancel safari yangu ya kwenda nchini China ili tu nihudhurie party hii ya Joti....nitasafiri siku mbili baada ya party hii" alisema Wolper.
Alipoulizwa kwamba ndoa yake ni lini? Wolper alimjibu mtangazaji kuwa masuala ya ndoa hawapangi wanawake bali suala hilo anamwachia mwanaume atakayemuoa.
No comments:
Post a Comment