BAD NEWS:AJALI YA GARI YAUA WAFANYAKAZI WA BANDARI HUKO ARUSHA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2017

BAD NEWS:AJALI YA GARI YAUA WAFANYAKAZI WA BANDARI HUKO ARUSHA

Taarifa mbaya zinaeleza kwamba kuna ajali ya kusikitisha imetokea mchana wa leo huko maeneo ya Usa River mkoani Arusha. Ajali hiyo imeondoka na maisha ya wafanyakazi wawili wa bandari.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kwamba dereva wa gari hilo ndugu Alfred Chijana aliyekuwa na gari lenye namba za usajili T.796 DFG Toyota Mark X alijaribu kulipita (overtake) gari lingine aina ya Noah akiwa katika mwendo mkali.

Gari katika kuipita Noah ndipo akaliparaza kidogo ubavuni na kukosa balansi na hatimaye Mark X ikaacha njia na kugonga mti mkubwa uliokuwa kandokando ya barabara kisha kupinduka. Ndani ya gari kulikuwa na abiria wawili ambao walipoteza maisha papo hapo.

Hapa chini ni baadhi ya picha za tukio hilo👇👇👇



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages