DIAMOND NA KUNDI LAKE WAKUTWA NA MAZITO....MSONDO NGOMA YAWADAI FIDIA YA MILIONI 300 ZA KITANZANIA...KISA KIZIMA KIPO HAPA CHINI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2017

DIAMOND NA KUNDI LAKE WAKUTWA NA MAZITO....MSONDO NGOMA YAWADAI FIDIA YA MILIONI 300 ZA KITANZANIA...KISA KIZIMA KIPO HAPA CHINI


Bendi ya muziki nchini Tanzania ya Msondo Ngoma, imemtaka msanii wa muziki wa bongo fleva, Diamond Platinumz pamoja na kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) liwalipe fidia kwa kuiga kionjo cha muziki uliopigwa katika nyimbo ya ‘Ajali’ bila idhini ya mmiliki.

Msondo Ngoma kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby (WCB) kuwalipa fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na kutumia kionjo hicho cha muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata idhini ya mmiliki.

Kionjo hicho kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye wimbo wa ‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.

Barua hiyo imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama wakishindwa basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages