FIFA YATANGAZA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUPANGA MAKUNDI KOMBE LA DUNIA 2018 - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 17, 2017

FIFA YATANGAZA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUPANGA MAKUNDI KOMBE LA DUNIA 2018


Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetangaza rasmi mfumo utakaoutumika kupanga makundi 8 ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi.

Tangazo hili limekuja muda mfupi baada ya timu ya taifa ya Peru kukamilisha jumla ya timu 32 zilizofuzu kushiriki michuano hiyo kwa kuifunga 2-0 New Zealand katika mechi yao ya pili ya mtoano iliyofanyika mjini Lima.

Droo ya upangaji makundi inatarajiwa kufanyika rasmi Disemba mosi mwaka huu mjini Moscow, ambapo timu shiriki awali zitaingia kwenye upangaji kwa kutatajwa kulingana na viwango vya ubora.


Mpaka sasa, Urusi ndiyo timu pekee iliyopangwa katika kundi na iko kundi A kwa kuwa mwenyeji wa mashindano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages