HARMORAPA AFUNGUKA KUHUSU KUMUOA WEMA SEPETU...NI BAADA YA DOGO JANJA KUFUNGA NDOA NA IRENE UWOYA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 4, 2017

HARMORAPA AFUNGUKA KUHUSU KUMUOA WEMA SEPETU...NI BAADA YA DOGO JANJA KUFUNGA NDOA NA IRENE UWOYA

Habari kubwa kitaa ni kuhusu Dogo Janja mtoto wa Ngarenaro kufunga ndoa na Irene Uwoya. Ndoa hiyo imezua maswali mengi huku watanzania wengi wakitoa dukuduku na wengine kufukua makaburi ya wanandoa hao.

Kitendo cha Dogo Janja na Uwoya kufunga ndoa kimemuibua msanii wa muziki hapa nyumbani Harmorapa ambaye hakusita kutoa pongezi zake huku akisisitiza wanadamu kuishi ndoto zao.

Harmorapa amempongeza Dogo Janja kwa ushupavu aliouonesha ambao umemuwezesha kufunga ndoa na msanii mkubwa kunako gemu ya Bongo muvi Irene Uwoya. Katika ujumbe wake alioutupia instagram Harmorapa amekumbushia kuhusu ndoto yake ya kumuoa Wema Sepetu.

"Sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja , naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake....Nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakuwa wangu" aliandika Harmorapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages