HII NI ORODHA KAMILI YA MAKADA MBALIMBALI KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WALIOJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI JANA JUMANNE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 22, 2017

HII NI ORODHA KAMILI YA MAKADA MBALIMBALI KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WALIOJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI JANA JUMANNE


 
Chama cha Mapinduzi (CCM) jana Jumanne katika Mkutano wa Kamati Kuu unaofanyikia Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kimepokea maombi ya kujiunga na chama hicho kutoka kwa makada mbalimbali wa vyama tofauti vya upinzani.
Pamoja na hayo, pia Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesoma hadharani barua ya maombi ya kurudishwa CCM ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Bi Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.

Makada kutoka vyama mbalimbali vya upinzani walioomba ridhaa ya kujiunga na CCM ni pamoja na Prof. Kitila Mkumbo, aliyekuwa Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo na wakili wa kujitegemea Albert Msando na Lawrence Kego Masha.

Wengine ni aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi, aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT-Wazalendo Samson Mwigamba pamoja na Katibu wa Kamati ya Programu za Kijamii Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Hlmashauri Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo Edna Sunga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti katika mkutano huo, makada hao wameeleza kuwa sababu zilizowapelekea kuvihama vyama vyao na kuomba kujiunga na CCM ni pamoja na kuridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Magufuli, CCM kuirudia misingi iliyowekwa na waasisi, juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi, nidhamu na uwajibikaji pamoja na jihudi za kutetea na kupambania maendeleo kwa wanyonge.

Makada hao wameahidi kuonyesha ushirikiano na kukitumikia CCM pamoja na kutoa ushauri katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuwashawishi wengine kujiunga na chama hicho pia.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa pamoja wameridhia kuwapokea wanachama hao wapya pamoja na kumsamehe Bi Sophia Simba aliyekuwa amefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages