Bilionea aliyeibuka ghafla hapa Tanzania Dkt. Louis Shika maarufu kama bilionea wa nyumba za Lugumi hii leo ameweka wazi kuhusu kampuni yake kubwa anayoimiliki. Dkt. Shika ameeleza hayo alipokuwa akihojiwa na chombo kimoja cha habari nyumbani kwake.
Ikiwa ni siku moja tangu aachiwe kwa dhamana kutoka polisi akituhumiwa kuharibu masharti ya mnada, mnada ambao ulihusu majumba ya kifahari ya Lugumi ukiendeashwa na kampuni ya Yono, Dkt. Louis amefunguka na kudai kwamba yeye siyo mbabaishaji.
Dkt. Louis amethibitisha kuwa yeye ni Rais wa kampuni ya Lance Fort kampuni ambayo inaonekana kuhusika na utengenezaji wa vitu mbali mbali na kampuni hiyo makao yake yapo jijini Moscow, Urusi.
"Ndugu mwandishi ingia hapo kwenye mtandao sachi www.lancefort.narod.ru kisha tazama hapo kwenye category ya Administration ndipo utaona kwamba Louis Shika ni nani kwenye kampuni hiyo" alisema Dkt. Louis.
Baada ya kuingia kwenye tovuti hiyo imeonekana kweli kampuni ya Lancefort ipo na inaendeshwa kutoka Moscow, Urusi huku rais wake akiwa ni Louis S Kid, Mkurugenzi mkuu ni Dr. Lunyalula KRS na Mkurugenzi mtendaji ni Butina Nataly Alexandrovna.
Hapa chini ni baadhi ya picha zilizochukuliwa kutoka kwenye tovuti hiyo ya www.lancefort.narod.ru




No comments:
Post a Comment