LOWASSA AFUNGUKA KUHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 22, 2017

LOWASSA AFUNGUKA KUHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa alisema jana Jumanne kuwa amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema .

Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages