
Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu hapa nchini marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoha amefunguka hisia zake na kudai kwamba Wema Sepetu ndiye mwanamke pekee aliyewahi kutambulishwa kwake kama rafiki wa mwanae. Hayo ameyasema wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Shilawadu kinachoruka kupitia televisheni ya Clouds.
Mama Kanumba ameenda mbali nakudai kwamba kama Kanumba angebahatika kupata mtoto na Wema Sepetu basi kwake ingekuwa ni furaha isiyo na kifani. Katika mahojiano hayo Mama Kanumba amemsifia Wema Sepetu kwamba ni mwanamke ambaye anampenda sana na tangu enzi za uhai wa Kanumba, Wema Sepetu amekuwa ni mwanamke mwenye staha na siku zote alikuwa akienda nyumbani kwa kina Kanumba akiwa kajivika dela.
Aidha mama Kanumba amefunguka kuwa Wema Sepetu ni mwanamke mwenye upendo na ni mwanamke mwenye kujali na kipindi ambacho alikuwa akienda nyumbani kwa Kanumba basi endapo akimkuta mama Kanumba anapika ama kuosha vyombo basi alikuwa akimsaidia hizo kazi.
"Yaani mwanangu kama angezaa na Wema Sepetu basi mimi ningefurahi sana...Wema Sepetu ni mwanamke ambaye nilikuwa nampenda sana na ni mwanamke ambaye siwezi kumlinganisha na mtu mwingine yeyote" alisema mama Kanumba.
No comments:
Post a Comment