MASHINDANO YA KIA MARATHON KUVUTIA UTALII WA NDANI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 20, 2017

MASHINDANO YA KIA MARATHON KUVUTIA UTALII WA NDANI


Mashindano ya KIA marathon yamefanyika jana Jumapili Novemba 19 katika uwanja wa kimataifa wa ndege KIA uliopo mkoani kilimanjaro na kushirikisha zaidi ya nchi 40 duniani kote.
Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa KADCO akizungumza na Mukama Funny Media
Hayo yamethibitisha na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO Bw. Christopher Mkoma ambaye ndiye msimamizi wa uwanja na kusema kuwa wameandaa mashindano hayo kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi yetu ili kuongeza pato la taifa kupitia utalii wa ndani.

Hata hivyo aliongeza na kusema kuwa kupitia mashindano hayo yamekua hamasa kubwa kwa wanariadha wa hapa nchini kwani wameweza kuchuana na wanariadha kutoka nchi mbalimbali ikiwemo kenya,uganda, afrika kusini na sudani.

Naye Meneja masoko wa KADCO Bi.Christina Mwakatobe ameyataka makampuni na Taasisi  mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano hayo  kwani wataweza kutangaza biashara zao na kuweza kuchangia kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii vilivyopo hapa nchini.


Meneja Masoko wa KADCO

Kwa upande wake Rais wa riadha nchini Mh. Antony Mtaka ameshukuru washiriki wote kutoka mataifa mbalimbali na kuwata watanzania kushriki zaidi na kushinda ili kuitangaza nchi
Baadhi ya Washiriki Wa mbio za Km 21 Wakiwa na Medani zao baada kumaliza Mbio

Rais wa Riadha Tanzania Bw. Antony Mtaka Akizungumza na waadishi wa habari




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages