NYOTA WA SOKA DUNIANI CRISTIANO RONALDO APATA MTOTO WA NNE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 13, 2017

NYOTA WA SOKA DUNIANI CRISTIANO RONALDO APATA MTOTO WA NNE

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo jana Jumapili amepata mtoto wa kike ambaye amemkamilishia idadi ya watoto wanne. Ronaldo amethibitisha hayo kupitia mitandao yake ya twitter na Instagram huku akionesha furaha isiyo kifani.

Nyota huyo wa Real Madrid ameiandikia dunia kuhusu mapokezi ya baby girl wake aliyemtambulisha kwa jina la Alana Martina ambaye amezaliwa akiwafuata mgongoni mapacha waliotua hapa duniani mnamo mwezi wa sita mwaka huu.

"Alana Martina amezaliwa, wote Geo na Alana wanaendelea vizuri! Sisi sote tunafurahi sana" aliandika Ronaldo kupitia mitandao yake ya Twitter na Instagram kwa kutumia lugha ya kireno.

Ronaldo kwa sasa anatimiza watoto wanne huku wawili wakiwa ni mapacha (kike) na (kiume). Mwanawe wa kwanza anafahamika kwa jina Cristiano Ronaldo Jr ambaye amezaliwa mwaka 2009 akifuatiwa na mapacha  Mateo Ronaldo na Eva Ronaldo na wawili hawa wamezaliwa mwezi Juni mwaka huu kupitia mama wa kizazi (Surrogate mother) na jana Jumapili Novemba 12 amezaliwa Alana Martina.
A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on




LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK YA MUKAMA FUNNY ILI UWE KARIBU NASI ZAIDI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages