RAIS MUGABE AKUTANA NA WAJUMBE WA SADC ILI KUWEKA MAMBO SAWA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 17, 2017

RAIS MUGABE AKUTANA NA WAJUMBE WA SADC ILI KUWEKA MAMBO SAWA


Serikali ya Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe amekutana na wajumbe kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( Sadc) katika juhudi za kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Alisafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi. Wanajeshi waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.

Duru zinadokeza kwamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika kwa uchaguzi mwaka ujao.

Lakini mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya taifa. Makamu wake wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Mzozo wa Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, nchini Botswana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages