Mama
mzazi wa msanii Wema Sepetu ambaye hapo jana ametangaza kurudi CCM, Bi,
Mariam Sepetu, amesema kitendo cha Wema kurudi CCM bila kumuomba
ushauri ni kitu ambacho kimemdhalilisha kama mzazi.
Mama
Wema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia
kitendo cha Mawanaye kurudi CCM, huku lawama nyingi zikiwa zinamuelekea
yeye kama mzazi kwa kutomshauri vema binti yake.
Akiendelea
kuzungumzia suala hilo, mama Wema amesema watu wanaomshauri Wema kama
wazazi wake si watu wazuri akimtaja Steve Nyerere, huku akisema hawana
mapenzi ya kweli na Wema kwani alipopata matatizo walimkimbia, na badala
yake CHADEMA ndio waliokuwa wakihangaika naye.
"Nasema
haya kuhusiana na Steve, Wema alipopata matatizo hakuweza kutokea
central kumuona Wema, leo anashangilia Wema kurudi CCM, lakini akumbuke
mimi nitabaki kuwa mzazi, CHADEMA walipoona nataabika nahangaika,
waliweza kuja mpaka nyumbani kwangu, kuja kutoa pole, wamemsaidia Wema,
napenda kusema CHADEMA ni familia moja, na nilijua kwamba kama
kunalolote Wema angerudi kutaka ushauri kwangu, hiki sio kitu chepesi,
ni kitu ambacho kimenidhalilisha, kimenitoa utu na najisikia vibaya",
amesema mama Wema.
Pamoja
na hayo mama Wema amesema Wema atabaki kuwa mtoto wake na hawezi
kumchukia kwa sababu ya kuhama chama, ingawa kitendo hicho kimemuumiza.
No comments:
Post a Comment