Heri ya Christmas ndugu msomaji na mtembeleaji wa ukurasa huu!!
Wakristo wote duniani leo hii wanaadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo. Ni sherehe ya aina yake ambayo inahitaji uangalifu mkubwa kiusalama na kiafya pia.
Mukamafunny blog hatuna mengi ya kusema zaidi ya kuwasisitiza watanzania na dunia nzima kwa ujumla kuwa waangalifu katika furaha hii hasa katika usalama wa watoto na makazi. Tunawakumbusha kama mtatoka kwenda kusherehekea basi hakikisha japo anabaki mtu mmoja nyumbani ili kuepusha vitendo vya wizi majumbani.
#Heri ya Christmas
#Tusherehekee kwa furaha na amani
#Tusisahau kuwakumbuka wenye uhitaji.
No comments:
Post a Comment