MWANAMKE AKAMATWA NA POLISI BAADA YA VIDEO YAKE KUSAMBAA AKIMVISHA MWANAMKE MWENZAKE PETE YA UCHUMBA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 1, 2017

MWANAMKE AKAMATWA NA POLISI BAADA YA VIDEO YAKE KUSAMBAA AKIMVISHA MWANAMKE MWENZAKE PETE YA UCHUMBA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtumishi wa mgodi wa GGM, Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Mfanyakazi huyo ambaye ni ofisa ugavi kitengo cha manunuzi anashikiliwa baada ya ‘video’ inayomwonyesha akimvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Video hiyo ambayo imezua mijadala hasa ikizingatia kwamba iko kinyume cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kwa uchunguzi kwa kuwa nchi hairuhusu mambo hayo.

Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.

#Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages