Wasanii wanaounda kundi la muziki la Navykenzo wamepata mtoto wa kiume na kumpa jina Gold. Tukio hilo la historia limetokea jana Jumamosi ambapo pia kwa Tanzania ilikuwa siku ya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru.
Navykenzo inayoundwa na wasanii wawili Aika &Nahreel ni kundi ambalo limedumu kwenye gemu ya bongo fleva huku pia uhusiano wa wawili hao ukionekana kudumu siku hadi siku mpaka hapo jana Mungu alipowatunuku mtoto wa kiume.
Wawili hao wamethibitisha ujio wa Gold kupitia kurasa zao za Instagram huku wakionekana na furaha ya aina yake.



No comments:
Post a Comment