RAIS MAGUFULI AMTEUA MWANASHERIA ALBERT MSANDO KATIKA TUME YA KUFUATILIA NA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NCHINI KOTE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 21, 2017

RAIS MAGUFULI AMTEUA MWANASHERIA ALBERT MSANDO KATIKA TUME YA KUFUATILIA NA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NCHINI KOTE

Mwanasheria Albert Msando amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa miongoni mwa watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini.

Albert Msando ameandika ujumbe huo wa shukrani kwenye ukurasa wake wa instagram, na kusema kwamba anaamini kazi hiyo itafanyika kwa weledi.

“Namshukuru Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wa kuwa mjumbe wa Tume ya Kufuatilia Mali za Chama. Chini ya uenyekiti wa Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na wajumbe wengine wa tume.Nnaamini kwa dhati kazi hii itafanyika kwa weledi ili kukiwezesha chama cha Mapinduzi kujitegemea kupitia mali zake”, ameandika Albert Msando

Hapo jana Rais Magufuli ameteuwa timu ya watu 9 ambao wataunda tume ya kufuatilia na kuhakiki mali za CCM nchini kote, baada ya kubaini kuna baadhi ya mali haziingizi kipato stahiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages