Shirika la ndege la kimataifa la Fly Dubai jana Ijumaa limeandika historia nyingine kwa kuzindua safari zake mpya kutoka Dubai kuja hapa Tanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro. Uzinduzi huo uliambatana na hafla fupi ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ambaye alisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO Mhe. Gregory Teu.
Naye Makamu wa rais mwandamizi wa shughuli za biashara wa fly dubai Bw. Sudhir Sreedharan ambaye aliongoza abiria pamoja na wahudumu wa ndege ya shirika hilo kutua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa KIA ameelezea furaha yake kutokana na jinsi ambavyo watanzania na Afrika kwa ujumla wataunganishwa na Dubai na kuwa kitu kimoja.
Pia bwana Sreedharan amezungumzia kuhusu bei ambazo zitakuwa rafiki kwa wateja wa Fly Dubai.
Aidha mgeni rasmi ambaye pia ni waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliwashukuru Fly Dubai kwa kuanzisha safari zao katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro kwani hii itakuwa ni fursa ya pekee ya kutangaza utalii wa Tanzania.
"Tunawashukuru wenzetu wa fly Dubai kwa kuanzisha safari zao hapa KIA kwani hii itasaidia kukuza utalii na biashara za hapa nchini kwenda katika mataifa yote ambayo ndege hii ya fly Dubai inapitia" alisema Profesa Mbarawa.
Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO Bw. Gregory Teu akihutubia wananchi katika hafla hiyo.
"Tunawashukuru wenzetu wa fly Dubai kwa kuanzisha safari zao hapa KIA kwani hii itasaidia kukuza utalii na biashara za hapa nchini kwenda katika mataifa yote ambayo ndege hii ya fly Dubai inapitia" alisema Profesa Mbarawa.
Makamu wa rais mwandamizi wa shughuli za biashara wa fly Dubai Bw. Sudhir Sreedharan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa fly Dubai.
Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO Bw. Gregory Teu akihutubia wananchi katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment