WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 17, 2017

WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu kupisha uchunguzi.

Katika taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa wizara ya ardhi Doroth Mwanyika imebainisha kumsimamisha Mchechu kwa mamlaka aliyopewa waziri Lukuvi kupitia kifungu F. 35 cha kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2009.

Waziri Lukuvi pia ametoa agizo kwa bodi ya Shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa huduma za mikoa na Utawala Raymond Mndolwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watendaji hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages