AJALI YAUA MMOJA NA KUJERUHI WATU WAWILI MKOANI KILIMANJARO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 20, 2018

AJALI YAUA MMOJA NA KUJERUHI WATU WAWILI MKOANI KILIMANJARO

Usiku wa jana Ijumaa kuna ajali mbaya ilitokea ikihusisha gari pamoja na pikipiki moja katika barabara ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA). Ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja jioni ambapo gari aina ya Jeep lenye namba za usajili T. 162 CAD liligonga pikipiki aina ya Toyo yenye namba MC. 293 BLT ambayo ilikuwa na abiria waliopakizana watatu (maarufu kama mshikaki).

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanadai kuwa gari hilo aina ya Jeep lilikuwa likitokea Mererani kwenda Arusha wakati lina-overtake gari lingine maeneo ya TANESCO-KIA ndipo likaigonga pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Njia panda KIA.

Ajali hiyo iliwajeruhi vibaya abiria wote watatu kwenye pikipiki na wakakimbizwa hospitali ya wilaya ya Hai na baada ya kufika huko abiria mmoja akapoteza maisha.

Ajali hiyo hadi hivi sasa iko mikononi mwa polisi na tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages