HATIMAYE KOREA KASKAZINI YARUHUSIWA KUPELEKA TIMU KOREA KUSINI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 10, 2018

HATIMAYE KOREA KASKAZINI YARUHUSIWA KUPELEKA TIMU KOREA KUSINI

Hatimaye Korea Kaskazini imeruhusiwa kupeleka wanamichezo wake kwenye mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi yatakayofanyika mwezi Februari nchini Korea Kusini.

Ruhusa hiyo imekuja baada ya kikao kizito cha majadiliano baina ya mataifa hayo ya peninsula kilichofanyika jana mjini Seoul.

Kizuizi kilichowekwa miaka miwili iliyopita baina ya mataifa hayo mawili cha wanachi kutembeleana na kuwasiliana kimeondolewa rasmi jana Jumanne.

Kuhusu ujumbe wa Olimpiki ya majira ya baridi. Korea Kaskazini imeruhusiwa kupeleka wachezaji, viongozi wa timu na mashabiki kwa ajili ya mashindano.


#CRI-Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages