
1. MR. BEAN:Huyu ni moja ya wachekeshaji maarufu duniani na majina yake halisi anaitwa Rowan Sebastian Atkinson. Mchekeshaji huyu alizaliwa Januari 6,1955 katika mji wa Consett nchini Uingereza. Baadhi ya filamu alizocheza Mr. Bean ni pamoja na Bean, Bean's Holiday, John English (2003) na John English Reborn ambayo ilitoka mwaka 2011.

2. WIZKID:Anaitwa Adoyeji Ibrahim Balogun mzaliwa wa nchini Nigeria. Amezaliwa tarehe 16 Julai 1990 katika mtaa wa Surulere, Nigeria. Kazi yake kubwa ni uandishi na uimbaji wa muziki. Pia Wizkid ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Boluwatife Balogun.

3. MC PILIPILI:Cheti chake kinasomeka Emmanuel Mathias mzaliwa wa Dodoma, Tanzania mtaa wa Airport. Pilipili alizaliwa tarehe 1 October 1985 akiwa ni mtoto wa pili katika familia ya Bwana Mathias Matebe na Bi. Mariam Matebe.

4. KCEE: Huyu ni mwanamuziki kutoka Nigeria. Anaitwa Kingsley Chinweike Okonkwo, amezaliwa tarehe 18 April 1979 katika eneo la Ajegunle, jijini Lagos, Nigeria. KCEE ni muimbaji, mwandishi, na mtumbuizaji katika masuala ya muziki na kazi hii ameifanya tangu mwaka 2013 hadi hivi sasa.

5. DAVIDO: Anaitwa David Adedeji Adeleke. Amezaliwa tarehe 21 November 1992, mjini Atlanta, katika jimbo la Georgia, nchini Marekani. Davido anajiingizia kipato kupitia kazi yake ya uandishi wa muziki, kurap, kutumbuiza na pia ni prodyuza japo haikufahamika ni studio gani anayoitumikia.
Ndugu msomaji, kwa ufupi hao ni baadhi ya wasanii na watu maarufu ambao wamekuwa wakifahamika kupitia majina yao ya kazini (Stage Names) na hii leo nimekufungua ubongo kuhusu majina yao halisi. Dondosha komenti yako na utuambie ni msanii au mtu gani maarufu ambaye ungependa nikufahamishe majina yake ya ubatizo (Kwenye cheti) nami ntamdadavua hapa hapa MUKAMAFUNNY BLOG.
No comments:
Post a Comment