Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 3, Januari, 2018 amehani msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola ambaye ni Mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola.
Kifo cha mke wa Mhe. Kangi Lugola ambaye pia alikuwa ni Kamishna Msaidizi wa Polisi Bi. Mary Lugola kilitokea juzi Jumatatu Januari Mosi jijini Dar es Salaam katika hospitali alipokuwa amelazwa kwa matibabu.


No comments:
Post a Comment