NI KWELI KWAMBA MIMI MARS ANATOKA NA JOH MAKINI????BASI SOMA HII UTAPATA MAJIBU YOTE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 30, 2018

NI KWELI KWAMBA MIMI MARS ANATOKA NA JOH MAKINI????BASI SOMA HII UTAPATA MAJIBU YOTE


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee, amefunguka tuhuma za kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rapper Joh Makini


Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Mimi Mars amesema yeye na Joh Makini ni sawa na mtu na kaka yake, kwani Joh Makini alikuwa rafiki kipenzi wa kaka yake.

“Mahusiano yangu mimi na Joh Makini ni ya kidada na kaka, kwa sababu Joh Makini ni mtu ambaye tumemjua kuanzia tukiwa wadogo, alikuwa rafiki yake kaka yangu mkubwa, kwa hiyo kama ambavyo kaka yetu mkubwa anatushauri ni sawa na Joh Makini, ni rafiki, ni kaka, ni mshauri, sijui suala la mahusiano limetoka wapi”, amesema Mimi Mars.

Mimi Mars amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote akikusudia kufocus kwenye kazi zake zaidi.
Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages