RAIS MUSEVENI AELEZA JINSI ANAVYOMPENDA TRUMP....AMEDAI KUWA MAREKANI IMEMPATA RAIS AMBAYE HAJAWAHI KUTOKEA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 24, 2018

RAIS MUSEVENI AELEZA JINSI ANAVYOMPENDA TRUMP....AMEDAI KUWA MAREKANI IMEMPATA RAIS AMBAYE HAJAWAHI KUTOKEA



Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitoa hotuba ambayo alitamka wazi alivyo na mapenzi makubwa kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Mapema mwezi huu Rais wa Marekani Donald Trump alituhumiwa kwa kutoa matamshi ya kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu kupindukia wakati wa mkutano wake na viongozi wa ndani wa taifa hilo waliokuwa wakijadili masuala ya uhamiaji.

Rais Trump amekanusha kutoa matamshi hayo lakini wabunge wa bunge la Senate waliohudhuria mkutano huo walisema kwamba alitoa matamshi hayo.Umoja wa Afrika ulimtaka Rais Trump kuomba radhi kwa matamshi ya hayo ya kibaguzi.

Lakini wakati Rais Yoweri Museveni akifungua mkutano wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) jijini Kampala alisema kwamba Marekani imempata Rais bora ambaye hajawahi kutokea huku kauli hiyo ikisindikizwa na vicheko kutoka kwa wabunge hao.

Rais Museveni alisema kwamba "Nampenda Trump kwa sababu anawaambia wafrika ukweli. Waafrika wanatakiwa kutatua matatizo yao wenyewe, waafrika ni dhaifu." alisema Museveni 


Rais Museveni alisema kwamba "Nampenda Trump kwa sababu anawaambia wafrika ukweli. Waafrika wanatakiwa kutatua matatizo yao wenyewe, waafrika ni dhaifu." alisema Museveni
Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages