Taarifa kutoka Momba mkoani Songwe zinaeleza kwamba askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani mwanaume ambaye jina lake halijawekwa wazi mwenye umri wa miaka 29 anadaiwa kumuua mpenzi wake kwa kumchinja na panga.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana Jumamosi Januari 6 jirani kabisa na kituo cha polisi Kamsamba kilichopo tarafa ya Kamsamba wilaya ya Momba mkoani Songwe ambapo askari huyo alikwenda kutekeleza unyama huo kwa mpenzi wake ambaye ni muuguzi katika kituo cha afya cha Kamsamba.
Baada ya ofisa huyo wa polisi kutimiza haja yake inasemekana kwamba alikuwa kazini katika kituo hicho cha Kamsamba na alikwenda katika ghala la silaha na kuchukua bunduki kisha kujipiga risasi ya shingo na maisha yake yakaishia hapo hapo.
Mtoa taarifa wetu anaeleza kwamba chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi ambapo askari polisi alikuwa akimtuhumu mpenzibwake huyo (nesi) kutokuwa mwaminifu na kuwa na mahusiano na wanaume wengine.
Tunaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu zaidi na taarifa ya polisi ikitolewa itakuwa na maelezo ya kina.

No comments:
Post a Comment