VIDEO: HIVI NDIVYO LOWASSA ALIVYOWATOA HOFU WANACHADEMA BAADA YA KUONEKANA NA GWANDA KWENYE KAMPENI KINONDONI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 27, 2018

VIDEO: HIVI NDIVYO LOWASSA ALIVYOWATOA HOFU WANACHADEMA BAADA YA KUONEKANA NA GWANDA KWENYE KAMPENI KINONDONI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amepokewa kwa nderemo na wafuasi wa chama hicho.

Lowassa ambaye kwa mara ya kwanza leo Jumamosi Januari 27,2018 amevaa gwanda tangu ajiunge na Chadema mwaka 2015 amewasili ofisi za chama hicho kanda ya Pwani zilizoko Magomeni, ambako yalianza maandamano kuelekea Mwananyamala ulikofanyika mkutano wa hadhara wa kampeni.

Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Ali Mapilau, Mwananyamala ambako kampeni zilizinduliwa.

Akizungumzia hatua ya Lowassa kuvaa Gwanda, Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Kinondoni, Rose Moshi amesema anadhihirisha kuwa ni kamanda na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi naye.

"Tulikuwa na hofu alipokwenda Ikulu, kuvaa kwake gwanda kunaonyesha kuwa ni mwenzetu," amesema.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Jerome Ulomi amesema Lowassa amedhihirisha kuwa ni mwana Chadema. Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages