
Gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) limegongana uso kwa uso na pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani (Trafiki).
Ambulance hiyo yenye namba za usajili DFP 8318 Toyota Land Cruiser mali ya halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ikiendeshwa na Charles Liyumba iligongana na pikipiki aina ya SANLG yenye namba MC.110 BGV iliyokuwa ikiendeshwa na askari mwenye namba H. 4729 PC Richard.
Tukio hili la kusikitisha limetokea hapo jana Jumanne majira ya saa nane mchana huko maeneo ya Mwembeni, kata ya Malinyi, wilaya Malinyi, mkoani Morogoro ambapo Ambulance hiyo ilikuwa ikitokea Mtimbira kwenda Malinyi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro afande Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Akizungumza na Mukamafunny Blog kamanda Matei amedai kuwa askari polisi alikuwa akitokea katika kituo cha polisi Malinyi kwenda eneo la kazi (check point) ndipo alipokumbwa na kadhia hiyo na kufariki dunia akipelekwa hospitalini Lugala kupatiwa matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendokasi wa Ambulance na kutochukuwa tahadhari kwenye eneo la kona ambapo dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi.
Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''
No comments:
Post a Comment