HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AKABIDHIWA LESENI ZA WASAFI FM NA WASAFI TV.....AWASHUKURU DK. SHEIN NA RAIS JPM - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 27, 2018

HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AKABIDHIWA LESENI ZA WASAFI FM NA WASAFI TV.....AWASHUKURU DK. SHEIN NA RAIS JPM

Ujio wa Wasafi Media ambazo ni Wasafi Tv na Wasafi Fm umekamilika hapo jana baada ya Diamond Platinumz, C.E.O wa Wasafi Classic Baby (WCB) kukabidhiwa leseni za vyombo vyake vya habari. Makabidhiano ya leseni hizo yamefanyika chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa Waziri wa Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Diamond amethibitisha hilo huku akitupia ujumbe wa shukrani kwa Rais wa Zanzibar pamoja na Rais John Pombe Magufuli.

"Leo tulikabidhiwa Rasmi Leseni ya @wasafitv na @wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni , Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma.....Shukran Nyingi ziifikie Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamuhuri nzima ya Muungano wa Tanzania... Ma raisi wetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison Mwakiyembe....Tamanio letu ni kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji ambao pengine hawajapata nafasi bado....kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi tusingekuwepo....lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni.... #HiiNiYetuSote"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages