JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI KWA GHARAMA NAFUU SANA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 22, 2018

JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI KWA GHARAMA NAFUU SANA

Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.

Mahitaji

Pumba ya mahindi sadolini 1.
Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
Dagaa sadolini 1.
Kilo moja ya soya.
Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.


Namna ya kuandaa

Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
Saga hadi zilainike.
Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
Anika kwenye jua la wastani.
Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.


Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages