KOREA KASKAZINI WANATAKA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAREKANI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 26, 2018

KOREA KASKAZINI WANATAKA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAREKANI

Korea Kaskazini ina nia ya kufanya mazungumzo na Marekani, kwa mujibu wa Korea Kusini. Tangazo hilo limekuja baada ya Jenerali Kim Yong-Chol kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kabla ya sherehe za kufungwa kwa mashindano ya olimpiki wa msimu wa baridi.

Binti ya rais wa Marekani Donald Trump Ivanka pia alihudhuria sherehe hizo, lakini maafisa wa Marekani wamekana kufanya mkutano na ujumbe kutoka Korea Kaskazini. Marekani inasema Korea Kaskazini ilijiondoa kutoka kwa mkutano na Makamu wa Rais Mike Pence wakati wa sherehe za ufunguzi.

Eneo la rasi ya Korea limegawanyika tangu vita vya mwaka 1950 hadi 1953 na pande hizi mbili hazijawahi weka sahihi mkataba wa amani. Uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Kusini umeonekana kama njama ya Korea kuvuruga ukaribu kati ya Korea Kusini na Marekani.

Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini. Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini.

Chanzo: BBC Swahili

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages