NAIBU SPIKA AMBURUZA MCH. MSIGWA KWENYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 9, 2018

NAIBU SPIKA AMBURUZA MCH. MSIGWA KWENYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE


Dk Tulia Ackson Mwansasu amempeleka Mbunge wa Iringa Mch Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration)

Tulia Ackson amesema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi. Kufuatia kauli hiyo ndipo hapo Naibu Spika aliagiza Mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili.

"Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi" alisema Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli Januari 31, 2018 alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages