TANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUMALIZA MVUTANO WA KIBIASHARA ULIOKUWEPO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 3, 2018

TANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUMALIZA MVUTANO WA KIBIASHARA ULIOKUWEPO

Kenya na Tanzania zimekubaliana kumaliza mvutano wao wa kibiashara, hivyo kufungua njia ya kuongeza maingiliano ya kibiashara ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

Nchi hizi mbili kubwa kiuchumi kwenye Soko la Pamoja la EAC zimekuwa na mvutano katika uhusiano wa kibiashara katika miaka michache iliyopita, ambao ulifikia kushuka kwa bidhaa za Kenya zinazoingizwa nchini Tanzania kwa asilimia 60 katika miezi ya mwanzo ya mwaka jana.

Katibu wa Kudumu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Chris Kiptoo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania Elisante Ole Gabriel wametoa waraka wa pamoja mjini Nairobi, Kenya siku ya jana wakisema, pande hizi mbili zimekubaliana kuondoa vikwazo vya bidhaa zisizotozwa ushuru.

Takwimu zilizotolewa na Utafiti wa Uchumi kwa mwaka 2017 nchini Kenya zimeonyesha kuwa, biashara kati ya Kenya na Tanzania inachangia zaidi ya asilimia 45 ya biashara yote ndani ya EAC.
Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages