WAZIRI MKUU MSTAAFU NCHINI BANGLADESH APIGWA JELA MIAKA MITANO - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 9, 2018

WAZIRI MKUU MSTAAFU NCHINI BANGLADESH APIGWA JELA MIAKA MITANO


Bi. Khaleda Zia-Waziri mkuu mstaafu wa Bang
Polisi nchini Bangladesh wamekabiliana na maelfu ya waandamanaji wanaopinga kufungwa jela miaka mitano kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Khaleda Zia kwa tuhuma za rushwa.

Bi Khaleda ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani amekana tuhuma za kutumia vibaya fedha za misaada ya kimataifa zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima nchini humo.

Kufuatia hukumu hiyo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72, hawezi kugombea katika uchaguzi wa Bunge utakaofanyika baada ye mwaka huu .

Hiyo ni moja ya mlolongo wa kesi zinazomkabili Bi. Khaleda ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Waziri Mkuu wa sasa Sheikh Hasina .

Kiongozi huyo anatuhumiwa kutumia vibaya Dola 252,000 zilizotolewa kwa ajili ya watoto yatima . Bi Khaleda alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke mwaka 1991 akiongoza chama cha Bangladesh Nationalist Party, BNP.

Kwa maoni na ushauri tuandikie kupitia mukamafunnyblog95@gmail.com au tuma ujumbe mfupi kwenda namba +255 (0) 768548171. Mukamafunny Blog>>"Habari na Burudani''

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages