MVUA KUBWA YATARAJIWA KUNYESHA KATIKA MIKOA YA KILIMANJARO, ARUSHA NA MANYARA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 1, 2018

MVUA KUBWA YATARAJIWA KUNYESHA KATIKA MIKOA YA KILIMANJARO, ARUSHA NA MANYARA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuanzia usiku wa leo Machi 1, 2018  hadi kesho Machi 2, 2018 kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo imebainisha maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro ambapo mvua hizo zitazidi milimita 50 ndani ya saa 24 huku ilieleza hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua.

TMA imewashauri wakazi wa maeneo husika kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages