Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic sasa rasmi ataihama timu hiyo na kuelekea kunako klabu ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani MLS.
Zlatan ambaye alijiunga na Man United 2016 kama mchezaji huru akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa, katika kipindi hicho akiwa Man United amefanikiwa kuifungia Man United magoli 29 katika michezo 53 wastani wa goli moja kwa mechi mbili, huku akitoa assist 9 na ameshinda mataji matatu.
Jeraha la goti la Zlatan limefanya aichezee United michezo saba pekee msimu huu na hajaichezea United toka Boxing Day katika mchezo dhidi ya Burnley iliyomalizika kwa Man United kupata sare ya kufungana magoli 2-2, taarifa rasmi inatajwa kuwa itatolewa siku zijazo lakini za chini ya kapeni zinaeleza kuwa Mourinho amempa baraka Zlatan ya kujiunga na LA Galaxy.
#Soka Kiganjani Blog
No comments:
Post a Comment