TFF YAMFUNGIA JOSEPH KANAKAMFUMU KWA MIAKA MITANO.....STORI KAMILI IKO HAPA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 1, 2018

TFF YAMFUNGIA JOSEPH KANAKAMFUMU KWA MIAKA MITANO.....STORI KAMILI IKO HAPA

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia kamati ya Maadili, limemfungia kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano Kocha maarufu nchini, Joseph Kanakamfumu kwa kosa la kugushi leseni za wachezaji.

Kanakamfumu amefungiwa akiwa kocha na mratibu wa timu ya Mvuvuma FC ya ligi daraja la kwanza.

Tuhuma zilizokuwa zikimkabili Kanakamfumu na wenzake wawili zilitokana na mechi namba 26 kundi A Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika Oktoba 29, mwaka jana kati ya Mvuvumwa FC na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo Mvuvumwa FC iliwachezesha wachezaji watano Elias Costa Elias (aliyekuwa amevaa jezi namba 5), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdala Dunia (jezi namba 1), Doto Justine Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba 8), ambao hakuwa na leseni halali.

Wengine waliokumbana na lungu la TFF ni Mwenyekiti na mmiliki wa timu hiyo Yared Fubusa pamoja na Katibu wa klabu hiyo Ramadhani Kimilomilo

"Kamati imemtia hatiani Kanakamfumu kwa makosa yote mawili, Kutoa taarifa za udanganyifu ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41(12) ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2017 na kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, Katika kosa la pili, Kanakamfumu aliamua kuwaongeza wachezaji hao baada ya kukabidhiwa timu kwa vile alifahamu uwezo wao na inaonekana alitumia uzoefu wake katika mpira wa miguu kupata leseni hizo za kugushi," ilisema taarifa ya TFF.

Adhabu hiyo iliyotolewa kwa Kanamfumu inatokana na kifungu cha cha 73 (7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

Aidha, kwa upande wa Fubusa, kamati imemkutana na makosa mawili likiwemo la kukaidi wito wa kamati iliyomuita kumuhoji, naye amefungiwa miaka mitano kwa kosa la kugushi leseni za wachezaji na mwaka mmoja zaidi kwa kukaidia wito wa TFF, na pia ametozwa faini ya shilingi 1,000,000.

"Kwa upande wa Kimilomilo, Kamati imemtia hatiani kwa kosa kushiriki kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73 (7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, Kimilomilo akiwa kama Mtendaji Mkuu wa Mvuvumwa FC alishindwa kusimamia timu yake ipasavyo na kusababisha ichezeshe wachezaji wasio na leseni.

Aidha Kimilomilo hakutoa taarifa TFF wala Bodi ya Ligi au kuchukuwa hatua zozote kwa Joseph Kanakamfumu licha ya kukiri mbele ya Kamati kuwa wachezaji hao hawakuwemo katika orodha ya Mvuvumwa FC.

Hii inamaanisha kuwa alishirikiana na viongozi wenzake kugushi leseni ili kuiongezea nguvu timu yake.," ilisema taarifa ya TFF.

Kwa makosa hayo, Kamati imemfungia Kimilomilo kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano.


#Nipashe

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages