THOBIAS OMEGA ATUNUKIWA CHETI CHA HESHIMA KUTOKA TAASISI YA ''WE CARE TANZANIA'' KWA KUSHIRIKI #NIOKOE NIISHI 2017 - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 21, 2018

THOBIAS OMEGA ATUNUKIWA CHETI CHA HESHIMA KUTOKA TAASISI YA ''WE CARE TANZANIA'' KWA KUSHIRIKI #NIOKOE NIISHI 2017



Mkurugenzi wa Taasisi ya WE CARE TANZANIA iliyopo Jijini Mbeya Bi. Elizabeth Maginga amemtunuku Cheti cha Heshima Ndugu Omega Thobias- Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Njombe. 

Bi. Elizabeth na Taasisi yake waliandaa Tamasha kubwa mwishoni mwa mwaka 2017 la kuhamasisha Jamii kuhusu Uchangiaji Damu salama kwa hiari kwa kusaidiana na Benki ya Taifa ya Damu Salama ambapo Bw. Thobias alishiriki kikamilifu. 

We Care Tanzania pia wamemtunuku Cheti hicho Miss Mbeya 2017 Miss Patricia Richard, Mshiriki wa Shindalo la Miss Mbeya 2017 Miss Evangelina Peter na Mchekeshaji maarufu Jijini Mbeya aitwaye Kashili (Chance Kashililika). 

Bw. Omega Thobias kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika hivi:- 

#NiweSautiYao Shukrani Taasisi ya @wecaretanzania kwa Kutambua Mchango wangu katika Kuhamasisha Jamii kuhusu Uchangiaji Damu salama kwa Hiari. 

Nilifanya kwa kujitolea kwani ni matamanio yangu kuwa Sauti Ya Watu wanyonge na wasio na sauti #NiweSautiYao 😘😘Nitaendelea kuwa Mpambanaji na Supporter mkubwa wa Movements zenye Tija kwa Jamii. #NiokoeNiishi 


Bw. Omega Thobias (mwenye kofia nyekundu) siku ya Tamasha la Niikoe Niishi Jijini Mbeya akiwa na Timu yake ya Hamasa kwa Jamii kujitokeza kuchangia Damu salama kwa hiari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages