TIMES FM WAOMBA RADHI KWA WANANCHI...NI KUFUATIA MAHOJIANO YAKE NA DIAMOND YALIYOZUA SINTOFAHAMU - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 29, 2018

TIMES FM WAOMBA RADHI KWA WANANCHI...NI KUFUATIA MAHOJIANO YAKE NA DIAMOND YALIYOZUA SINTOFAHAMU


Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kilichorusha mahojiano ya mwanamuziki Diamond Platnumz kimeomba radhi kwa kauli tata zilizozua mjadala nchini.

Taarifa hiyo iliyowekwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ilisema imeamua kuomba radhi kutokana na kauli tata alizotumia msanii huyo wakati akihojiwa katika kipindi cha Play List kinachoongozwa na mtangazaji Omary Tambwe.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba siku hiyo Diamond alialikwa katika kipindi hicho kwa ajili ya kupongezwa kwa kumpa tuzo maalumu nyota wa mchezo kwa mchango wake kwenye muziki na kutoa ajira kwa vijana.

Jingine ni kutangaza lugha ya Kiswahili kupitia muziki na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia sanaa ya muziki na kutoa albamu yake mpya ya ‘A Boy From Tandale ‘ ambapo kituo hicho kilimtaja kama msanii bora wa kiume, msanii bora wa kimataifa kwa kuvunja rekodi na msanii mwenye ushawishi zaidi na pia kumpatia tuzo maalum (Plaque).

“Kwa namna ambayo haikutarajiwa , mwanamuziki huyo alitumia kauli tata dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika mahojiano hayo.

“Uongozi wa Times unaomba radhi kwa Wizara, Naibu Waziri, TCRA, Basata pamoja na umma kutokana na kauli hiyo ya Diamond kwani Times haikuwa dhamira yetu kwa sintofahamu hiyo na tumekuwa tunafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za utangazaji,” imesema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages