WAKILI AELEZA KUHUSU HALI YA AVEVA....ADAI KUWA AMELAZWA ICU-MUHIMBILI - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 8, 2018

WAKILI AELEZA KUHUSU HALI YA AVEVA....ADAI KUWA AMELAZWA ICU-MUHIMBILI

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Hayo yameelezwa leo Machi 8 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na wakili anayewatetea, Evodius Mtawala wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo.

“Mshtakiwa wa kwanza Aveva, tangu jana amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi hali yake siyo nzuri," ameeleza wakili Mtawala.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai naye ameliambia mahakama kuwa Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Mtawala ameiambia mahakama kuwa walizungumza na upande wa mashtaka wataeleza jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wameomba wapewe siku 14 ili waweze kueleza kitu.

Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Machi 22, 2018.

Wakati kesi hiyo ikitajwa mahakamani hapo alikuwapo Godfrey Nyange maarufu Kaburu ambaye ni makamu wa rais wa Klabu ya Simba.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa kiasi hicho cha fedha.

Washtakiwa hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages