BAKWATA YATANGAZA MABADILIKO KATIKA UPATIKANAJI WA VIONGOZI WAKE....VIONGOZI WOTE WATATEULIWA BADALA YA KUCHAGULIWA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 6, 2018

BAKWATA YATANGAZA MABADILIKO KATIKA UPATIKANAJI WA VIONGOZI WAKE....VIONGOZI WOTE WATATEULIWA BADALA YA KUCHAGULIWA


Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limefanya mabadiliko ya upatikanaji wa viongozi kwa nchi nzima kuanzia ngazi ya Masheikh wa wilaya, mikoa na Taifa.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la BAKWATA kikao kilichokaa Mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi Machi, Mufti alisema wamekubaliana kwa kauli moja kuwa upatikanaji wa viongozi wa Kiislamu utakua ni wakuteuliwa na sio kuchaguliwa tena kama ilivyo sasa.

Amesema Mkutano Mkuu uliofanyika Machi 31 - Aprili 1 umesema kuwa mfumo wa uchaguzi hauwaachi watu salama sana sana husababisha migogoro ya hapa na pale na makundi yenye kuleta chuki na kwamba mfumo wa kuteua ndiyo mfumo wa kiislam

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikh Khamis Mataka amesema mbali na utaratibu huo wameanzisha mfumo mmoja wa kukusanya mapato ili kukusanya fedha hizo kwa umakini tofauti na ukusanyaji wa sasa ambao una mapungufu mengi na kupoteza baadhi ya mapato.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages