MBUNGE ATAKA ZANZIBAR KUWA MWANACHAMA EAC - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 4, 2018

MBUNGE ATAKA ZANZIBAR KUWA MWANACHAMA EAC

Mbunge wa Kojani, Hamad Salim Maalim (CUF) amehoji ni lini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaruhusu Zanzibar kuwa na uwakilishi rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiuliza swali leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu, mbunge huyo amedai hatua hiyo ni kwa kuwa mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar yanaitambua Zanzibar kuwa ni nchi.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustino Mahiga amesema Ibara ya pili (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mabadiliko yake imebainisha eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar. Pia ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

“Naomba kulihakikishia bunge kuwa maslahi yote ya Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yanazingatiwa ipasavyo,” amesema Mahiga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages