MWANDISHI PASCAL MAYALLA NA WAHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA MATATANI....NI BAADA YA KUANDIKA HABARI YA KULIDHARIRISHA BUNGE, SPIKA AAGIZA WAHOJIWE - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 12, 2018

MWANDISHI PASCAL MAYALLA NA WAHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA MATATANI....NI BAADA YA KUANDIKA HABARI YA KULIDHARIRISHA BUNGE, SPIKA AAGIZA WAHOJIWE


Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, inatarajia kuwahoji mwanahabari Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la kila wiki, la Raia Mwema kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge, Aprili 9 wiki hii.

Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.

Hayo yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?” haidhalilishi bunge.

Spika Ndugai leo Aprili 12, ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages