Rais wa zamani wa Korea Kusini amehukumiwa miaka 24 jela - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 6, 2018

Rais wa zamani wa Korea Kusini amehukumiwa miaka 24 jela



Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye, amehukumiwa miaka 24 jela baada ya kukutwa na hatia katika matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha nchi kushuka kiuchumi.

Park Geun-hye aliondolewa madarakani mwaka jana baada ya kutuhumiwa kutumia vibaya wadhifa wake na kusababisha kuanguka kwa uchumi.

Rafiki yake Choi Soon-sil, anayehusishwa na kashfa hiyo, alihukumiwa wiki mbili zilizopita hadi miaka 20 jela kwa kupokea hongo iliyotolewa na makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na makampuni yai Samsung na Lotte.

Katika mashtaka yake, mwendesha mashtaka alimshtaki rais wa zamani kuwa “alisababisha mgogoro wa kitaifa kwa kuacha mtu ambaye hajawahi kushiriki katika usimamizi wa umma kuongoza nchi”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages