UBUYU:KIKWETE AKUTANA NA ALI KIBA....ABARIKI NDOA YA MSANII HUYO, PICHA ZOTE ZIKO HAPA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 15, 2018

UBUYU:KIKWETE AKUTANA NA ALI KIBA....ABARIKI NDOA YA MSANII HUYO, PICHA ZOTE ZIKO HAPA

Ukisikia mambo ni moto basi usifikiri ni utani. Usemi huu unathibitika baada ya taarifa mbali mbali kusambaa zikidai kuwa mzee wa 'Seduce Me' Ali Kiba anatarajia kuvuta jiko (kuoa).

Hapo jana Ali Kiba amemtembelea rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambapo matembezi hayo yamehusisha pia mpango wake wa kuoa hivi karibuni. Rais Kikwete ameeleza kupitia Instagram kuhusu kufurahishwa na maamuzi hayo mazuri kwa Kiba.

"Namshukuru @OfficialAliKiba kuja kunitembelea na kunitaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni. Nimempatia nasaha zangu na kumtakia kila la kheri kwa jambo hilo jema aliloamua kufanya" aliandika rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Naye Ali Kiba hakusita kuelezea furaha yake kuhusu kukutana na Jakaya Kikwete ambapo kupitia ukurasa wake wa Insta Kiba aliandika:-

"It was nice to see you and your beautiful family Muheshimiwa @jmkikwete Mwenyezi MUNGU Awajaalie Afya Njema
#KingKiba"




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages