WOLPER NA SARAH WA HARMONIZE WAKINUKISHA INSTA.....KISA PENZI LA KONDEBOY, MAPOVU YAMWAGWA YAKUTOSHA - MUKAMAFUNNY BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 10, 2018

WOLPER NA SARAH WA HARMONIZE WAKINUKISHA INSTA.....KISA PENZI LA KONDEBOY, MAPOVU YAMWAGWA YAKUTOSHA



Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper na Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

Baada ya kutolewa povu hilo, Wolper alimrudishia kombora hilo Sarah na kuandika maneno haya:

Hii sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages