Aliyekuwa
Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia leo
Jumatatu Desemba 4, 2017 amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) mapema leo katika ofisi za chama hicho.
==>YALIYOSEMWA NA MAULID MTULIA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA KADI YA CCM LEO
“Nimejivua
nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa
navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya
sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli.
“Mimi
ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee. Nimejiunga na CCM
ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli. Nimetoka
kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani,
haki na Demokrasia ya kweli. Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya
mengi makubwa zaidi,” alisema Mtulia.
“Sijaja
CCM kutafuta cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya kujiunga
na chama chochote kile ninachokitaka. Kila jambo nililokuwa namwomba
Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa)
ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa.
“Nawashangaa
Viongozi wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali na shughuli
za Bunge, hizo shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo wanawasusia
wenye mamlaka? Nipo tayari kuwa hata Balozi wa nyumba kumi na
ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani Rufiji.
“Nawahaidi
wana CCM watafurahia uwepo wangu na watanufaika nami ndani ya CCM.
Nawaambia wana Kinondoni wasikosee, wachague Mbunge anayetokana na CCM.
Wachague CCM siku zote,” alisema Mtulia
IMETOLEWA NA;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa.
No comments:
Post a Comment